Waathiriwa wa Mkasa wa Boti Tudor Creek Bado Wanalia Haki

0
100

Ni miezi mitatu baada ya mkasa wa boti uliotokea katika eneo la Tudor Creek, Bahari Hindi, waathiriwa na familia za waliopoteza maisha bado wanalalamikia kutengwa na kupuuzwa licha ya ahadi mbalimbali zilizotolewa na mamlaka husika.

Mkasa huo ulitokea wakati wa mashindano ya ocean festival ambapo boti iliyokuwa imewabeba washiriki ilipata hitilafu na kuzama, na kusababisha vifo vya watu huku wengine wakiwa ni manusura.

Baada ya tukio hilo, serikali na wadau mbalimbali waliwaahidi waathiriwa msaada wa kifedha, matibabu pamoja na fidia kwa familia za waliopoteza wapendwa wao. Hata hivyo, waathiriwa wanasema kuwa ahadi hizo hazijatekelezwa kikamilifu, hali iliyowaacha wengi wakiendelea kuteseka kisaikolojia na kiuchumi.

Mkasa huo ulitokea wakati boti iliyokuwa ikishiriki katika mashindano ya Ocean Festival ilipokumbwa na mkazo na kutumbukia, ikisababisha vifo vya watu watatu na majeraha kwa washiriki wengine. waathiriwa na familia sasa wakidai kutengwa, licha ya ahadi zilizotolewa na mamlaka kuwasaidia kupata haki za wapenda wao.

Lydia Anyange mamake Tom Wanyonyi aliyefariki katika mkasa huo anasema kwamba Tom ndiye aliyekuwa tegemezi katika familia hiyo akisema mkasa huo unamuumiza hadi sasa.
Alex okumu ni mmoja wa manusura ambaye ameeleza kwamba tangu mkasa huo waratibu wa sherehe hiyo ya ocean festival hawajaweza kufika kusema hata pole kwa familia zilizoathirika na mkasa huo.

“Sisi ni wanyonge tungeomba kilio yetu isikike sisi tunachoomba ni haki ipatikane,” alisema Alex

Kwa sasa, waathiriwa wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa Haki Afrika wakili Yusuf Abubakar wamesema watachukua hatua za kisheria iwapo maafikiano ya moja kwa moja hayatafua dafu. Shirika hilo limesema litawasaidia waathiriwa kufuatilia fidia, kuwawajibisha waliokuwa na jukumu la kuhakikisha usalama, na kuhakikisha kuwa sauti za waathiriwa zinasikika.

“Kulingana na uchunguzi wetu kuna utepetevu ulifanyika wakati wakupanga hayo mashindano kwa mujibu wa sheria kuna ridhaa inafaa ipatiwe wale walofariki na wale waloathirika kwa namna moja ama nyingine”Alisema Yusuf

Waathiriwa sasa wanaitaka serikali kuingilia kati kwa dharura, kutimiza ahadi zilizotolewa, na kuweka wazi ripoti kamili ya uchunguzi wa mkasa huo. Pia wanataka hatua madhubuti zichukuliwe ili kuzuia majanga kama hayo kutokea tena siku zijazo.

 

LEAVE A REPLY