Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeingia katika tuhuma kali mapema mno kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
Barua iliyotolewa na chama cha DCP ikiangazia madai mazito dhidi ya Naibu Mwenyekiti wa IEBC, Bi. Fahima Araphat Abdallah, imefungua mjadala mzito kuhusu uaminifu wa taasisi ambayo inapaswa kuwa nguzo kuu ya demokrasia ya taifa.
Tahariri inasema leo kwamba si wakati wa kupuuzia simu za tahadhari. Huu ni wakati wa kusimama kidete na kuuliza maswali ya msingi ambayo yanaamua hatima ya nchi.
Kwa kawaida, matatizo ya IEBC huibuka miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu, si miaka miwili mapema. Kwa hivyo, hali ya sasa inamaanisha jambo moja tu kuna hitilafu za kimfumo ambazo zimeota ndani ya tume, na ikiwa hazitadhibitiwa, zitaathiri uchaguzi wa 2027 kwa ukubwa ambao unaweza kuitikisa Kenya.
Wakati Naibu Mwenyekiti wa IEBC anatajwa kwenye tuhuma za Kuingilia uchaguzi mdogo, Kuwatisha maafisa wa uchaguzi,Kushirikiana na wanasiasa kupanga matokeo Kupokea na kupanga mazingira ya utoaji wa rushwa,hii si tu hoja ya kisiasa ni kitisho cha moja kwa moja kwa uhuru wa uchaguzi na uadilifu wa kitaifa.
Ikumbukwe kwamba Nafasi ya Naibu Mwenyekiti sio ya mzaha Huyu si afisa wa kawaida wa serikali Ni mtu anayeshika usukani wa mchakato mzima wa uchaguzi Anajua taratibu za tume,Anafahamu mianya ya udhaifu, Anashika siri za ndani ambazo zinaamua kushinda au kushindwa kwa taifa.
Kwa hivyo, tuhuma dhidi yake si uzushi wa barabarani ni maumivu yanayochoma moyo wa demokrasia. Ikiwa madai haya yana chembe ya ukweli, basi tume ina doa hilo mapema mno.
Nisiseme sana IEBC imetaja kutumia zaidi ya KSh 700 milioni kuendesha chaguzi ndogo 22. Ni kwangu na kwako, Mkenya wa kawaida, tunalipa kodi nzito bila huruma ili tume iwe huru, yenye uadilifu, na isiyoweza kutikiswa.
Lakini je, ina maana gani kutumia mamilioni ikiwa matokeo yanaweza kurekebishwa kwa mikutano ya hotelini usiku?
Je, tume inawezaje kuhalalisha matumizi haya ikiwa maafisa wake wanaweza kuvuruga uchaguzi kwa ushawishi wa wanasiasa?
Tume inayodai kuwa huru inapaswa kujibu mara moja, kwa uwazi, kwa maelezo, na kwa uthabiti sio kwa kujikunyata kana kwamba hakuna kinachoendelea.
Ukiona taasisi muhimu inakaa kimya, basi ujue kwamba
Uhalisia wa madai unakuwa mzito zaidi kuliko ukimya unaotolewa.
swali kuu ambalo mkenya anajiuliza na kujijibu ni kwamba je IEBC inaweza kuaminiwa na kutoa jibu la HAPANA ‘ IEBC haiwezi kuaminiwa bila hatua madhubuti.Ikiwa tume inaweza kuacha tuhuma kubwa kiasi hiki zizunguke bila ufafanuzi.
Kutoka kwa meza hii ya tahariri nitasema kwamba tume zauchunguzi EACC DCI wafanye uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi mara moja na waweze kutoa habari hadharani bila hivyo kuamini tume hii itakuwa ngumu mno kuliko ngumu yenyewe.TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA



