Ni Lini Tutakuwa na Demokrasia ya Kweli?

0
106

Katika miaka ya karibuni, tumeshuhudia mataifa mengi ya Afrika yakifanya chaguzi lakini je, hizi kweli ni chaguzi za kidemokrasia, au ni tamasha la kisiasa lililojaa vumbi la jeuri, hofu na udanganyifu? Je, bado tunaweza kuziita “sherehe za demokrasia” wakati wananchi wanajawa na hofu badala ya matumaini?

‎Katika za Afrika nchi Hususan Tanzania, Kenya, na mataifa mengine mengi, mara kwa mara tumeyaona mazingira ya kisiasa yakifunikwa na wingu zito la vurugu, vitisho, kukamatwa kiholela na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.‎Tumeona polisi wakipewa amri badala ya maadili, na kutumia katiba polisi wanatumia nguvu kubwa kupita kiasi kutekeleza wajibu ambao wamepatiwa na mkenya kwenye katiba.

‎Viongozi wengi wamegeuka kuwa wakali na madhalimu, wakitumia sheria, vifungu, na vyombo vya usalama kama silaha za kulinda madaraka badala ya kulinda demokrasia.

‎Upinzani mara nyingi unakuwa si rafiki wa mabadiliko bali unachukuliwa kama adui wa taifa. Tunashuhudia watu wakipigwa, wakinyanyaswa, wakitekwa, wakitishwa, na mara nyingine hata kupotezwa. Haya yote yanajengwa juu ya kisingizio cha “kulinda amani”. Lakini amani gani inayojengwa juu ya unyang’anyi wa uhuru?

‎Katika baadhi ya nchi, mamlaka ya polisi na vyombo vya usalama yanaongezwa bila uwajibikaji. Mara nyingi, askari wanawajibika kwa maagizo kutoka juu badala ya misingi ya sheria na haki. Wananchi wanabaki wanyonge wakishuhudia haki ikipotea mbele ya macho yao, huku sauti zao zikizimwa kama mshumaa katika upepo mkali.

‎Ukweli mchungu ni kwamba demokrasia katika mataifa mengi ya Afrika bado inategemea hiari ya watawala, sio nguvu ya taasisi. Inaonekana kama jambo linaloweza kuimarishwa au kudidimizwa kulingana na maslahi ya walio mamlakani. Watakaonufaika na udhaifu wa mifumo hukataa kuijenga, wakati wanaoathirika na udhaifu huo wanabaki kupiga kelele bila kusikika.

‎Tutafika lini mahali ambapo chaguzi zitakuwa za kweli, sio maigizo?

‎Tutafika lini ambapo chama tawala hakitaogopa upinzani?

‎Tutafika lini ambapo polisi hawatatumika kama mkono wa kisiasa?

‎Tutafika lini ambapo kuikosoa serikali hakutakuwa sawa na kujitia hatarini?

‎Tutafika lini ambapo kura moja ya raia itakuwa na uzito kuliko maamuzi ya mtu mmoja aliye juu?

‎Ni lini tutaweza kusema kwa uhakika kwamba Africa has finally arrived kwamba tumefikia demokrasia ya kweli, uhuru wa kweli, na utawala wa sheria unaomlinda kila mmoja?

LEAVE A REPLY