Mombasa ,KENYA
Katika juhudi za kuhakikisha kila mkazi wa Kaunti ya Mombasa anapata huduma bora ya maji safi, Gavana wa Mombasa Abdulswammad Nassir amezindua rasmi kampeni ya siku 100 ya kutokomeza miunganisho haramu ya maji, uharibifu wa miundombinu, na wizi wa maji unaoigharimu kaunti hiyo kiasi kikubwa cha maji kila siku.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Gavana alieleza kuwa kilio cha wananchi kuhusu upungufu wa maji kimesikika, na serikali ya kaunti imechukua hatua madhubuti kulitatua tatizo hilo.
”asilimia sitini ya maji yetu yanaibiwa tukonkatika hali wa juu zaidi katika kenya huku kwetu kwa wizi wa maji”Alisema gavana nassir
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, asilimia 60 ya maji yanayozalishwa Mombasa hupotea kupitia wizi, uvujaji na uharibifu wa miundombinu hali hii inamaanisha kwamba kwa kila lita 10 za maji, lita 6 hazifiki kwa wananchi.
Kaunti ya Mombasa inahitaji takriban mita za ujazo 200,000 za maji kila siku, lakini ni mita 40,000 pekee ndizo zinazopatikana. Hata hivyo, kutokana na wizi wa maji, kinachowafikia wananchi ni kiwango cha mita 20,000.
Katika operesheni ya awali iliyofanyika maeneo ya Junda, Mwakirunge na sehemu za Kisauni, maafisa wa kaunti kwa kushirikiana na idara ya afya ya umma, walibaini miunganisho haramu 21 ya maji. Cha kusikitisha, baadhi ya waliohusika ni maafisa wa serikali ya kaunti na wengine wa serikali kuu.
”kuna baadhi ambao wamefanya miunganisho haramu wengine watu wanafanya jazi kwa serikali ,na wengine ni wafanyakazi wa kaunti hatua itachukuliwa bila kujali wewe ni nani”Alisema gavana Nassir
Gavana alitoa wito kwa wakazi wa Mombasa kushiriki kikamilifu kwenye mapambano haya ya wizi wa maji na kuripoti mtu yeyote anayefanya miunganisho haramu ya maji aidha gavana aliahidi kuzindua nambari ya simu maalum kwa ajili ya kuripoti visa hivyo, na wananchi watakaotoa taarifa zitakazosaidia watapokea zawadi kama motisha.



