Magavana Na Mfumo Mpya Wa E-Procument

0
141

Tumewaona magavana wakiitisha mkutano wa dharura baada ya rais william ruto kutangaza kuleta mfumo mpya wa kutafuta zabuni za serikali E PROCUMENT tunafaa tujiulize mbona magavana wameonekana na ghadhabu nyingi na kukataa mfumo huo tunafaa tujiulize Je, ni kweli wanafanya hivi kwa maslahi ya wananchi wa kaunti zao, au kuna maslahi yao binafsi yanayotishiwa? Kwa nini mfumo wa e-Procurement, unaolenga kuleta uwazi na haki katika utoaji wa kandarasi, unaonekana kuwa tishio kwao?

Niseme wazi kwamba kwa muda mrefu, viongozi wengi wa serikali za kaunti na hata serikali kuu wamezoea mfumo wa zabuni usio na uwazi. Je, si kweli kwamba kandarasi nyingi zimekuwa zikitolewa kwa kampuni ambazo zina uhusiano wa karibu na viongozi hawa? Na je, si huu ndio mfumo ambao umeendeleza ufisadi na kuhujumu maendeleo katika kaunti zetu?

Iwapo mfumo wa e-Procurement utatekelezwa ipasavyo, itamaanisha kuwa magavana hawa hawatakuwa tena na uwezo wa “kuchagua” ni kampuni gani ipate zabuni? Je, hawahofii kupoteza udhibiti wao wa zabuni ambazo wamekuwa wakizitumia kama njia ya kujinufaisha kisiasa na kifedha?

Na iwapo kama wataonekana kuukubali mfumo huu kwa nje, sharti tujiulize ni mbinu gani mpya watatafuta ili kuendeleza ulaji kwa njia ya kificho? Je, mfumo huu mpya una uwezo wa kuziba mianya yote ya hila na ujanja? ama utakuwa kama mifumo mingi ambayo tumeiona ikifadhiliwa kwa ushuru wa mwananchi kama E CITIZEN SHA NEMIS na mengine mingi ambazo hadi leo zimekuwa na ujanja

Rais William Ruto amesisitiza nia yake ya kupambana na ufisadi. Lakini je, ataweza kusimama kidete dhidi ya upinzani mkali kutoka kwa viongozi walio ndani ya mfumo wake mwenyewe?Najiuliza tu kwamba rais anaweza kubali kukabiliana na magavana waliodhamiria kuvuruga mchakato huu wa mageuzi kwa sababu maslahi yao binafsi yanaguswa ama atawahifadhi katika mifumo tufouti kwa manufaa ya kisiasa ya 2027?

 

LEAVE A REPLY