Je,vita Dhidi Ya Ufisadi Bado Viko?

0
100

Serikali ilipotangaza kuanza rasmi vita dhidi ya ufisadi, Wakenya wengi walipata matumaini mapya. Rais mwenyewe akatangaza na kuahidi hadharani kwamba hatalegeza kamba katika mapambano dhidi ya ufisadi, akisisitiza kuwa wale wote watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria. Maneno hayo yalikuwa matamu masikioni mwa wananchi waliotamani kuona haki ikitendeka na mali ya umma ikilindwa.

Hata hivyo, kama ilivyo kawaida katika historia ya taifa letu, maneno mengi mazuri yamesemwa lakini matendo machache yamefuata. Wakenya wakatapata walichotarajia cha kawaida UKIMYA. Tangu enzi za watawala wa jadi hadi sasa, kauli kuhusu kupambana na ufisadi zimekuwa zikirejelewa mara kwa mara, lakini vitendo halisi havionekani.

Hivi karibuni tulimsikia Waziri wa afya Aden Duale akiahidi kwamba wale wote waliohusika katika sakata ya mabilioni ya pesa katika Shirika la Huduma kwa Afya (SHA) watachukuliwa hatua kali.akasema kwamba atawataja badala ya majina hayo kutajwa hadharani, akadai ameyawasilisha kwa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI). Tangu wakati huo, kimya kimezagaa, na wananchi hawajasikia lolote kuhusu hatua zilizochukuliwa.

Bungeni nako, kumekuwa na minong’ono kuhusu rushwa. Wengine wanasema hakuna, wengine wanadai ipo hali inayoonyesha kwamba bado kuna utata na upungufu wa uwazi katika idara mbalimbali zinazofaa kuwakilisha mwananchi.

Serikali iliyopita ilikiri wazi kuwa takribani shilingi bilioni mbili hupotea kila siku kutokana na ufisadi. Aidha, tumeshuhudia baadhi ya magavana wakifunguliwa kesi za ubadhirifu wa fedha katika kaunti zao, huku maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) wakifanya misako. Lakini kesi hizo mara nyingi huisha kimyakimya, na wananchi hubaki bila majibu.

Dalili zinaonesha kwamba bado kuna muingiliano na utata mkubwa kuhusu uhuru wa idara zinazopambana na ufisadi na ufanisi wao EACC imelaani ODPP kwa kutoka kwa kesi kubwa za ufisadi waliopewa na EACC na baadaye ODPP zikachukuliwa au kuacha bila hukumu. Kwa mfano, EACC ilisema kuwa hadi 18 kesi za juu za rushwa zimeondolewa kwa ODPP bila matokeo.

Ripoti zinaonyesha kuwa idara kama Directorate of Criminal Investigations (DCI) na ODPP hazina rasilimali za kutosha, au miundo ya ndani ya kufanya kazi ya uchunguzi na mashtaka inakosa ufanisi.

Idara za Nchi kama marekani na nchi zingine zilizoendelea huwa zinafanya kazi kwa upekee na bila muingiliano kutoka kwa serikali kuu na hata idara nyingine , na tukija nchi yetu?
Katika kulinganisha, katika nchi kama United States idara za usalama na uchunguzi kwa mfano Federal Bureau of Investigation (FBI)) zinajitegemea na zina uhuru mkubwa na zinajisimamia bila kuingiliana sana kutoka idara moja kwa moja. Katika Kenya, bado kuna mgongano wa mamlaka, utata wa utekelezaji, na idara nyingi zikiashiria kushindwa kwa migogoro ya ndani.Nitasema mgogoro wa ‘Mtu mkuu” au ufungaji wa kesi unapendelea kutokea, kwa maana hakuna “boss” aliyechukuliwa hatua kwa mfano mkubwa na wazi. Wale wanaoshikwa ni wa hongo za hapa na pale lakini wale BOSS Wamejificha ofisini wakipigwa na kiyoyozi na kunywa kahawa moto inayolipiwa na ushuru wa mwananchi.

Nitasema kwamba ikiwa serikali iko nqa dhumuni la kweli la kupigana na ufisadi sharti tuone wafisadi wale wanaojiita maBOSS na BIGFISH wakifikishwa mahakamani na kuhukimiwa wakenya wamechoka kelele za mdomo bila vitendo.

LEAVE A REPLY