Profesa Kithure Kindiki Ndiye Naibu Rais Mpya Wa Kenya

0
122
Prof. Kithure Kindiki aapishwa kuwa naibu rais Novemba 1, 2024

Nairobi, KENYA

Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Profesa Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa naibu rais mpya wa Kenya.

Kithure Kindiki anachukua mahala pake Rigathi Gachagua aliyeondolewa madarakani.

Kindiki anachukuwa wadhfa huo baada ya siku kadhaa za makabiliano mahakamani baina ya mawakili wa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na wale wa serikali.

Gachagua alienda mahakamani kuzuia Kindiki asiapishwe baada ya kudai kwamba aliondolewa madarakani kinyume na sheria.

Hafla ya kumwapisha Kindiki imefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.

Taarifa ya gazeti la serikali kuhusu hafla hiyo ilitolewa saa chache tu baada ya Mahakama kuu kuondoa agizo la lililomzuia Prof. Kindiki kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.

“Inaarifiwa katika taarifa ya umma kwamba hafla ya kumwapisha Naibu Rais mteule itafanyika Ijumaa, Novemba 1, 2024, katika ukumbi wa jengo la kimataifa la mikutano la Kenyatta (KICC) katika kaunti ya Nairobi, kuanzia saa nne asubuhi. ,” ilisema taarifa ya gazeti la serikali iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau.

Hii inakuja baada ya Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua kupata pigo, Mahakama ya rufaa ya Kenya ilipokataa kutoa maagizo ya kuizuia Mahakama kuu kuendelea na kesi hiyo dhidi yake iliyohusu kumuondoa madarakani.

LEAVE A REPLY