Rais William Ruto Aongoza Makala Ya 61 Ya “Mashujaa Day” Kaunti Ya Kwale

0
110
Rais William Ruto akikagua gwaride la heshima katika uwanja wa michezo wa Kwale katika hafla ya Mashujaa Day, Jumapili, Oktoba 20, 2024

Kwale, KENYA

Rais William Ruto Jumapili Oktoba 20, 2024 aliongoza Wakenya wakati wa sherehe za 61 za Mashujaa katika Uwanja mpya wa michezo katika Kaunti ya Kwale.

Maelfu ya Wakenya kutoka sehemu mbalimbali za nchi walianza kuwasili katika uwanja huo, mapema saa tano asubuhi.

Kulingana na serikali ya kaunti ya Kwale, uwanja huo ambao hafla hiyo ya kitaifa iliandaliwa una uwezo wa kukimu hadi watu elfu 10.

Usalama uliimarishwa ndani na karibu na uwanja huo, huku maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) na Huduma ya Kitaifa ya Polisi wakitumwa kutoka Kombani hadi Kwale mjini.

Rais aliandamana na mkewe Rachel Ruto, Naibu Rais mteule Kithure Kindiki, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi, na Gavana wa Kwale Fatuma Achani.

 

 

LEAVE A REPLY