Rais Ruto Amteua Profesa Kithure Kindiki Kuwa Naibu Rais

0
94
Profesa Kithure Kindiki

Nairobi, KENYA

Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais baada ya Rigathi Gachagua kuvuliwa mamlaka na bunge la Senate Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limewasilishwa Bungeni ambapo wabunge watalipigia kura.

Spika Moses Wetang’ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa Ijumaa.

“Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais kuhusu uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kujaza nafasi katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya,” Wetang’ula alitangaza.

Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo.

“Prof. Kindiki, ambaye hadi uteuzi huo amekua akihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kushika nafasi ya Naibu Rais.

Bunge lazima lipigie kura ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina hilo.

Baada ya kuidhinishwa, atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake.

Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.

LEAVE A REPLY