Maseneta Nchini Kenya Wamuondoa Afisini Naibu Wa Rais Rigathi Gachagua

0
104

Nairobi, KENYA

Maseneta wa Kenya wamepiga kura ya kumuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua ofisini licha ya kushindwa kutoa ushahidi wake katika kesi ya kumuondoa madarakani baada ya wakili wake kusema kuwa amepelekwa hospitalini.

Katika moja ya siku za kushangaza katika historia ya hivi majuzi ya kisiasa nchini Kenya, Gachagua alipaswa kufika katika Seneti baada ya chakula cha mchana kujitetea, siku moja baada ya kukanusha mashtaka 11.

Hata hivyo, Gachagua, hakufika na wakili wake akaomba kesi iahirishwe akisema mteja wake alikuwa akisumbuliwa na ‘maumivu ya kifua’ na alikuwa akitibiwa na madaktari katika Hospitali ya The Karen.

Ilipotimu saa kumi na moja jioni Gachagua hakuweza kufika bungeni.

Maseneta kisha waliamua kuendelea na kesi bila Gachagua kuwepo, na hivyo kusababisha  mawakili wake kuondoka bungeni.

Maseneta vile vile walikataa pendekezo la kuchelewesha kesi hiyo hadi Jumamosi hatua iliyoonesha jinsi walivyodhamiria kumuondoa Gachagua, miezi kadhaa baada ya kutofautiana na Rais William Ruto.

Wiki iliyopita, idadi kubwa ya wabunge katika Bunge la Kitaifa walipiga kura kuunga mkono hoja ya kumuondoa Gachagua mamlakani, na kuweka msingi wa kesiya siku mbili katika Seneti.

LEAVE A REPLY