Bunge la Bunge La Seneti Kenya Kupiga Kura Kuhusu Hoja Ya Kumuondoa Madarakani Naibu Rais

0
83
Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Nairobi, KENYA

Bunge la Seneti nchini Kenya linatazamiwa kupiga kura Alhamisi Oktoba 17, 2024 kuamua iwapo litamuondoa Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani katika mchakato wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Kenya.

Bunge la Seneti litatoa uamuzi wake katika siku ya pili ya kesi dhidi ya Naibu huyo wa Rais.

Hii inafuatia kura ya kihistoria iliyopigwa wiki iliyopita katika bunge la kitaifa, kumshtaki Gachagua kwa mashtaka 11 yakiwemo ufisadi, uasi, kuidhoofisha serikali na kutekeleza siasa za kugawanya taifa kikabila.

Kesi katika Baraza la Seneti ilianza Jumatano baada ya Gachagua mwenye umri wa miaka 59, kushindwa katika jitihada nyingi za mahakama kusitisha mchakato huo.

Anatarajiwa kutoa ushahidi atakapojitetea mbele ya seneti siku ya Alhamisi.

LEAVE A REPLY