Gaza, PALESTINE
Mapigano yanaendelea huko Gaza, ikiwa ni pamoja na Jabalia kaskazini, ambapo vifaru vya Israel na wanajeshi wanafanya operesheni ya ardhini.
Katika taarifa Alhamisi, jeshi la Israel limesema limeshambulia maeneo 45 ya Hamas huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, ikiwa ni pamoja na kambi za Hamas.
Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza imesema zaidi ya Wapalestina elfu 42 wameuawa katika mashambulizi ya kijeshi ya Israel tangu yalipoanza mwaka mmoja uliopita.
Hilo ni ongezeko la watu 45 kwa jumla eikilinganishwa na siku iliyotangulia.
Wizara haitofautishi kati ya vifo vya wapiganaji kutoka Hamas na raia, inapochapisha takwimu hizo.
Israel imetoa amri ya watu kuhama kaskazini mwa Gaza, lakini Philippe Lazzarini kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) anasema watu elfu 400 wamenaswa katika mapigano.