Bunge Lote La Seneti Kusikiliza Hoja Ya Kumuondoa Mamlakani Naibu rais Rigathi Gachagua

0
76
Moja ya vikao vya bunge la seneti la Kenya.

Nairobi, KENYA

Bunge la Seneti limetupilia mbali pendekezo la kuunda kamati maalum ya watu 11 kuchunguza mashtaka ya hoja iliyopitishwa na bunge ya kum-bandua mamlakani Naibu Rais Rigathi Gachagua yaliyo.

Pendekezo hilo lilitolewa na Kiongozi wa Wengi Aaron Cheruiyot Jumatano ambaye alisema kuwa kamati hiyo ingekuwa na jukumu la kuchunguza mashtaka dhidi ya DP Gachagua na kuwasilisha matokeo yao kwa Seneti kwa mahojiano zaidi.

“Ninataka kuwasihi wanachama wakubaliane nami kwamba tuchague Maseneta 11 wetu wenye busara na wanaoaminika zaidi ambao tunafikiri wana hekima ya kutosha kusoma kwa niaba yetu na kufanya uamuzi,” alisema Cheruiyot.

Pendekezo hilo hata hivyo halikuungwa mkono na baadhi ya maseneta kwani Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna alisema kuwa suala hilo limevutia wananchi na linastahili kushughulikiwa na bunge lote kwa pamoja.

Spika wa Seneti Ammerson Kingi alibainisha kuwa suala hilo litashtakiwa katika kikao cha pamoja.

Aidha, aliagiza kuwa mwaliko wa kufika mbele ya Seneti ufanywe kwa Naibu rais Gachagua, Bunge la Kitaifa na pande zinazohusika katika hoja ya kumtimua.

Pande hizo zitatarajiwa kuwasilisha ripoti zao kufikia Jumatatu, Oktoba 14 na Seneti itachunguza suala hilo Jumatano na Alhamisi.

Spika Kingi pia aliwaonya Maseneta dhidi ya kujadili suala hilo hadharani ili kuhakikisha matokeo ya haki yatapatikana watakapolijadili.

“Tuache kutoa maoni hadharani kuhusu hoja hii. Kufanya hivyo ni kutarajia mjadala ambao utakiuka Kanuni za Kudumu. Alisema Kingi.

Wajumbe wa bunge la kitaifa, Jumanne walipiga kura kumtimua Gachagua  baada ya hoja iliyowasilishwa kujadiliwa kwa siku nzima huku wabunge 281 wakiunga mkono kumuondoa naibu huyo wa rais mamlakani, 44 wakipiga kura kupinga hoja hiyo na mbunge mmoja  hawakupiga kura.

 

 

LEAVE A REPLY