Hoja Ya Kumuondoa Madarakani Naibu Wa Rais Wa Kenya Yaanza Kujadiliwa Bungeni

0
81
Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Nairobi, KENYA

Bunge la Kitaifa nchini Kenya limeanza kujadili hoja ya kumuondoa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.

Wabunge wameanza kujadili hoja hiyo Jumanne Oktoba 8, 2024 baada ya Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse kuwasilisha sababu 11 kupitia hoja ya kutaka kumuondoa madarakani mnamo tarehe 26 Septemba.

Naibu wa rais Rigathi Gacagua anatarajiwa kujitetea Jumanne jioni baada ya wabune kumaliza kujadili hoja hiyo.

Gachagua amekana shutuma zote dhidi yake katika kikao na wanahabari siku ya Jumatatu.

Mchakato huo umeanza kwa kuwasilisha ripoti ya zoezi lililoshirikisha umma lililoendeshwa kutoa maoni kuhusu hoja ya kumuondoa naibu huyo wa rais mamlakani ambapo Wakenya walitoa maoni yao kwa kila tuhuma 11 zinazomkabili Gachagua.

Iwapo hoja hiyo itapata uungwaji mkono wa thuluthi mbili bungeni yaani wabunge 233 ya kati ya 349 basi itawasilishwa kwa bunge la Seneti.

Hata hivyo ikiwa wabunge 117 wataikataa, naibu wa rais atasalia madarakani.

LEAVE A REPLY