New York, MAREKANI
Zaidi ya watu 100 wanatarajiwa kumshtaki mwanamuziki wa rap Sean ‘Diddy’ Combs maarufu kama P. Diddy, kwa unyanyasaji wa kingono, ubakaji na vile vile kutumiwa vibaya kingono.
Wakili wa Texas Tony Buzbee amesema baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathiriwa ni pamoja na watoto wadogo ambao yasemekana walinyanyaswa walipokuwa na umri wa miaka tisa.
“Hili ni jambo muhimu ambalo tunakusudia kulifuatilia kwa uzito,” wakili Buzbee aliwaambia waandishi wa habari.
Wakili anayemwakilisha P. Diddy, Erica Wolff anasema rapa huyo anakanusha madai hayo, akisema ni “uongo na yenye lengo la kumharibia sifa”.
Awakili huyo alisema yeye na wenzake “watafanya kila wawezalo kuwapata wahusika ” katika madai ya unyanyasaji, au “mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ilishiriki au kufaidika na tabia hii ya kuchukiza”.
Hatua hiyo ya kisheria ni ya hivi karibuni dhidi ya P. Diddy.
P. Diddy alikamatwa wiki iliyopita na anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu ya ulanguzi wa ngono na biashara ya ngono.
Kwa sasa yuko chini ya ulinzi baada ya kunyimwa dhamana, ambayo anasema anakata rufaa.
Madai hayo ya unyanyasaji wa ngono yamegonga vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni hasa Afrika mashariki.
Baadhi ya wasanii wa nyimbo ambao walishawahi kufika Marekani na kukaribishwa na rapper P. Diddy wamekua wakiandamwa na maswali kuhusu iwapo walidhulumiwa kingono.