Nairobi, KENYA
Seneta wa Makueni Daniel Maanzo amewasilisha hoja ya kujadili utendakazi wa Rais wa Kenya William Ruto.
Hoja hiyo imewasilishwa katika bunge la Seneti wakati bunge la kitaifa likianza mchakato wa kumuondoa madarakani naibu wake Rigathi Gachagua.
Hoja ya Maanzo, inayoangazia ukiukaji wa katiba unaodaiwa kufanywa na rais, iliwasilishwa huku polisi wakiimarisha usalama nje ya Bunge na katikati mwa jiji la Nairobi.
Hoja hiyo inamshtumu Ruto kwa kukosa kulinda Wakenya, ikiangazia ukosefu wa usalama wakati wa maandamano ya vijana wa GenZ mwezi Juni, ambayo yalikuwa maandamano ya kupinga Mswada tata wa Fedha.
Seneta huyo wa Makueni pia anamktoa wito wa kumshinikiza rais kutekeleza sera muhimu katika sekta ya elimu na afya bila kuwashirikisha Wakenya kikamilifu.
“Rais William Ruto amewatenga baadhi ya Wakenya na anaendelea kuzidisha mivutano kati ya sekta tofauti kutokana na sera zake tata,” Maanzo alisema.