Mgombea Urais Tunisia Ahukumiwa Miaka 12 Jela

0
74
Bango lenye picha ya mgombea urais aliyehukumiwa miaka 12 jela, Ayachi Zammel.

Tunis, TUNISIA

Mgombea uraisi kwa tiketi ya upinzani nchini Tunisia Ayachi Zammel amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka manne, likiwemo la kuiba kura zilizomuidhinisha kuwa mgombea wa urais.

Wakili wa Zammel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado mwanasiasa huyo anabakia kuwa mgombea katika uchaguzi huo wa rais utakaofanyika siku ya Jumapili (Oktoba 6).

Zammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kiliberali na ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tunisia kupambana na Rais Kais Saed katika uchaguzi huo wa rais.

Tume ya uchaguzi imewazuia wagombea wengine 14 kuwania katika uchaguzi huo.

(Habari hii ni kwa hisani ya DW)

LEAVE A REPLY