Ushuru Mkubwa Unaokusanywa Huelekezwa Kwa Kulipa Madeni

0
205
Msimamizi wa bajeti Margaret Nyakango

Nairobi, Kenya

Ripoti ya msimamizi wa bajeti imedhibitisha kuwa asilimia 83 ya ushuru unaokusanywa na serikali hutumiwa kulipa madeni.

Msimamizi wa bajeti Margaret Nyakango amesema shilingi trilioni 4.18 mwaka wa kifedha  2022/23, zilitumiwa kulipa madeni, huku serikali ikiwachwa na asilimia 17 pekee kuendesha shughuli zingine.

Hii ina maana serikali italazimika kukopa Zaidi ili kuendeleza miradi yake.

Mamlaka ya mapato nchini KRA inatarajiwa kukusanya shilingi trilioni 2.7 ifikapo mwisho wa mwaka wa kifedha ya 2023/2024 na asilimia kubwa ikitarajiwa kutumiwa kulipa madeni.

Nyakango  pia ameeleza hofu kuhusu utumiaji wa fedha za matumizi ya kila siku kwa serikali zote  akisema inazidi kudhihirisha utumiaji mkubwa wa fedha ya umma.

Ametoa mfano wa shilingi trilioni 3.6 zilizotengewa serikali kuu na asilimia 38 zilizotumiwa kulipa mishahara na marupurupu.

Ameongeza kuwa shilingi bilioni 20 zilitumiwa na watumishi wa umma katika safari za nje na za ndani.

Amehimiza serikali kuendeleza miradi yake kulingana na mapato yake.

LEAVE A REPLY