Meru, Kenya
Rais Wiliam Ruto kwa mara nyingine ameonya viongozi watakaojihusisha na ufisadi humu nchini kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Rais Ruto anasema serikali yake haitawapa nafasi watu watakaorejesha nyuma maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika ziara yake kaunti ya Meru Rais rais Ruto pia ameonya viongozi mbalimbali kuweka kando tofauti zao za kisiasa ili kufanikisha maendeleo kwa wananchi.
“Wale wanaota ndoto kwamba wataiba mali yetu, ama watatumia ufisadi na ukora na utapeli, kuharibu mali wakenya wametafuta, ushuru wakenya wamelipa, hawa watu nimewaambia mambo yao hayatafaulu.” alisema rais Ruto.
Amehimiza viongozi kuangazia maendeleo ya kaunti zao kwani katika uchaguzi wa 2027, wananchi watakuwa nafasi ya kuwatambua waliotimiza ahadi zao au kuzembea ofisini.
Ziara ya Rais Ruto kaunti ya Meru inajiri huku malumbano yakishuhudiwa baina ya viongozi kaunti hiyo ya karibuni yakiwa malumbano baina ya gavana Kawira Mwangaza na Naibu wake Isaac Mutuma.