Wakenya Zaidi Ya Milioni 3 Huvuta Bangi

0
205

Nairobi, Kenya

Kenya imeorodheshwa nafasi ya sita kwa idadi ya watu wanaovuta bangi barani Afrika.

Kulingana na utafiti wa kitengo cha Afya na Elimu cha Marekani, Kenya ina waraibu milioni 3.3 wa bangi.

Nigeria ndiyo iliyo na watu wengi barani afrika ambao ni waraibu wa bangi.

Utafiti huo unaonesha watu milioni 20.8 ni waraibu wa bangi nchini Nigeria.

Ethiopia ndiyo ya pili ambapo raia milioni 7.1 huivuta huku Misri ikiwa na watu milioni 5.9 ambao ni waraibu wa mihadarati hiyo.

Taifa la DR Congo limeorodheshwa la nne Afrika likiwa na wavutaji milioni 5, Tanzania ikiwa na wavutaji milioni 3.6.

Taifa la Sudan liko katika nafasi ya saba kwa kuwa na wapenda bangi  milioni 2.7 huku taifa la Uganda likiwa na wavutaji milioni 2.6.

Madagascar iko na waraibu wa bangi milioni 2.1 nayo Ghana ikiwa ya 10 kwa kuwa na waraibu milioni 2.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa yam waka wa 2021 ilionesha kwamba wavutaji bangi Afrika walikuwa wakiongezeka kwa kasi na huenda wakafika asilimia 40 kabla ya mwaka 2030.

Marekani, Canada, Nigeria na Australia zimetajwa kuongoza kwa waraibu wa bangi kote duniani.

Katika mataifa hayo, waliorekodiwa kupenda bangi sana ni walio na umri wa kuanzia miaka 15.

Zimbabwe, Malawi, Niger na Zambia ni mataifa yaliyo-orodheshwa  kuwa na idadi ndogo ya waraibu wa bangi wakiwa ni milioni 1.1, 1.2, 1.2 na 1.4 mtawalia.

Hata hivyo, ripoti hizo zote zinaonya kwamba uraibu wa bangi ni hatari kwa afya ya watumizi na athari kuu Zaidi ikiwa ni matatizo ya akili kwa binadamu.

LEAVE A REPLY