Omanyala Amezea Mate Dhahabu Katika Mashindano Ya Dunia, Budapest

0
149
Ferdinand Omanyala

Bingwa wa mbio za Jumuiya ya Madola za mita 100 Ferdinand Omanyala amelinganisha “ushindani” wa mbio za mita 100 na ndondi huku akilenga dhahabu kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia mwezi huu huko Budapest.

Omanyala ataingia katika mji mkuu wa Hungary baada ya kujipatia ushindi wake wa kwanza wa mbio a Diamond League mwezi Julai.

Omanyala wa umri wa 27, aliibuka mshindi katika mashindano ya Monaco mbele ya Letsile Tebogo wa Botswana, aliyeshikilia rekodi ya dunia ya mita 100 miongoni mwa vijjana, huku Wajamaika Ackeem Blake na Yohan Blake wakiwa wa tatu na wa nne mtawalia.

Sasa Omanyala  anasema yuko tayari kuingia kwenye jukwaa la kimataifa katika riadha anayosema inavutia watu wengi zaidi kama vile ilivyo kwa ndondi.

“Mita 100 ni maarufu zaidi kwa sababu ya kelele zake – naiona kama mechi ya ndondi. Katika mechi ya ndondi, kuna mbwembwe za kila aina ikiwemo vyombo vingi vya habari na (mbio za mita 100) ni kama sekunde tisa za ushindani. Kwa wanariadha wa 100m, naweza kusema ni wa hali ya juu sana – wenye bidii kupita kiasi – ndio maana tunaufanya mchezo kuwa wa kuvutia.” Omanyala aliambia BBC Sport Africa.

Akiwa mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika, baada ya kukimbia sekunde 9.77 mwaka wa 2021, Omanyala alitwaa dhahabu kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2022 mjini Birmingham alipokimbia kwa sekunde 10.02.

Baada ya kuweka rekodi bora zaidi ya mita 100 mwaka huu – 9.84s nyumbani Nairobi wakati wa Mashindano ya Kip Keino Classic mnamo mwezi `Mei – Omanyala sasa analenga kumaliza wa kwanza katika mbio za mita 100 katika mashindano ya dunia.

 

LEAVE A REPLY