Watu watatu hawajulikani waliko baada ya gari walimokuwa wakisafiria kuvamiwa na washukiwa wa al-shabaab Jumanne asubuhi katika eneo la Koreni barabara ya Lamu kuelekea Garsen.
Magari kadhaa ya uchukuzi wa umma yaliyokuwa yakitokea Mombasa kuelekea Lamu pia yamevamiwa.
Gari moja aina ya Toyota Probox limepigwa risasi mara moja.
Watu wawili waliokuwa kwenye gari hilo wamepatikana wakiwa salama.
Gari lingine lililojaribu kugeuka ili kukwepa, limekosa mwelekeo na kuingia msituni na watu watatu waliokuwa ndani hawakupatikana kwa haraka.
Magari mengine yaligeuka na kukatiza safari zao.