Gavana Gideon Mung’aro: Zabuni Na Kandarasi Kufaidi Mwenyeji Wa Kilifi

0
228

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro anasema zabuni za kaunti sasa zitapewa wenyeji wa Kilifi.

Gavana Mung’aro amesema atabadilisha baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali ya awali kwa lengo la kumfaidi mkaazi wa Kilifi.

Anasema wakati zabuni zitatolewa, watakaozingatiwa kwanza ni wale walio karibu na eneo ambalo mradi utaendeshwa.

Amedokeza kuwa kwa miaka mingi zabuni za miradi ya kaunti zilipewa  watu wanaotoka nje ya Kilifi  na hivyo fedha inaishia kuendeleza kaunti zingine.

Gavana Mung’aro amesema serikali yake itashirikiana na wazee wa mitaa na machifu kufuatilia wanaotuma maombi ya kutaka kandarasi au zabuni.

Gavana Mung’aro  vile vile ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika serikali yake katika wiki chache zijazo, ili kuboresha huduma zinazotolewa huku akiwaonya wafanyikazi wa kaunti dhidi ya kuzembea kazi.

Amesema serikali inapanga kuanzisha mfumo wa kidigitali wa (Biometric) kubaini wafanyakazi wanaokwepa kuingia kazini.

LEAVE A REPLY