Serikali Ya Kijeshi Niger Kumshtaki Rais Aliyeondolewa Madarakani

0
149

Niamey, Niger

Jeshi la Niger linasema litamfungulia mashitaka ya uhaini, rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Msemaji wa jeshi la Niger amesema rais Bazoum amefanya uhaini mkubwa na kudhoofisha usalama wa ndani na nje wa nchi.

Bazoum wa umri wa miaka 63 na familia yake wamezuiliwa katika makazi rasmi ya rais huko Niamey tangu mapinduzi ya Julai 26.

Rais aliyeondolewa madarakani amesema matibabu ambayo yeye na familia yake wamepokea ni “ya kikatili” lakini serikai ya kijeshi ilisema baada ya daktari kumtembelea Bazoum kwamba hakukuwa na matatizo yoyote kuhusu afya yake.

LEAVE A REPLY