Wahudumu Wa Mochari Wamkemea Inspekta Jenerali Japheth Koome

0
159

Muungano wa wasimamizi wa makafani umepinga matamshi ya inspekta Generali wa polisi Japhet Koome kwamba viongozi wa upinzani walikodisha miili ya watu kutoka kwa hifadhi za maiti wakati wa maandamano ya kupinga serikali.

Muungano huo unasema matamshi hayo yanadhalilisha utendakazi wa wahudumu  makafani licha ya wao kujitolea kuhudumia wakenya kwa haki.

Muungano huo wa wahudumu wa sehemu za kuhifadhia maiti unasema inasikitisha kwamba afisa wa hadhi kama ya Koome, anaweza kutamka matamshi kama hayo bila kutathmini athari zake kwa huduma wanazotoa.

Wameambia wanahabari kwamba wametumia muda mrefu kuinukia na mikakati ya kuboresha huduma zao lakini matamshi ya Koome yanaonekana kama ya kutaka kuwarudisha walikotoka.

Sasa wanasema ikiwa Inspekta generali wa Polisi Japhet Koome ana ushahidi kuhusu madai hayo basi auweke wazi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Na endapo atakosa kufanya hivyo, aombe radhi na kufuta matamshi hayo kwa wafanyakazi wa makafani na pia kwa umma.

Mapema wiki hii Inspekta Generali wa polisi Japhet Koome alituhumu viongozi wa upinzani kwa kuenda katika makafani na kukodi miili ya watu kwa misingi kuwa polisi walitumia nguvu kupita kiasi na hata kuua watu  wakati wa maandamano.

LEAVE A REPLY