Mahakama ya Shanzu mjini Mombasa imeagiza kiongozi tata wa dini Paul Mackenzie na watu wengine 27 wazuiliewe kwa siku 47 zaidi.
Mackenzie na wenzake tayari wamezuiliwa na polisi kwa zaidi ya siku 90.
Jumanne iliyopita mkurugenzi wa mashtaka aliwasilisha ombi la kutaka Mackwnzie azuiliwe kwa siku 47 zaidi kuruhusu polisi wamalize uchunguzi dhidi yake.
Wakili wa Mackenzie Wycliff Makasembo akapinga ombi hilo akisema upande wa mashtaka umeshindwa kumfungulia mteja wake mashtaka.
Lakini hakimu mkuu wa mahakama ya Shanzu Yusuf Shikanda si sawa kuwaachia washukiwa kabla ya kutathmini wanakoelekea.
Shikanda ametilia shaka mahali watakakokwenda endapo angewaachia huru kwani eneo wanakotoka la Shakahola limetajwa kuwa la kuogofya.
Mackenzie anahusishwa na mauaji ya watu 400 waliokuwa washirika wa kanisa lake kwa madai ya kuwashawiki wakatae kula kama njia moja ya kufika mbinguni haraka.
