Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameondolewa hukumu ya miezi 15 jela .
Hukumu hiyo imeondolewa kufuatia agizo la rais Cyril Ramaphosa la kuwaondolea hukumu wale waliohukumiwa kwa makosa madogo madogo.
Wafungwa wengine zaidi ya elfu 9 wameachiwa huru kufuatia msamaha huo wa rais.
Mahakama ya Rufaa iliyomhukumu Jacob Zuma awali imekosoa msamaha huo ikisema umekiuka sheria.
Waziri wa sheria Ronald Lamola amesema uamuzi huo ulichukuliwa ili kushughulikia wafungwa wengi katika magereza na kwamba mchakato huo ulianza mwezi Aprili.
Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 mwaka 2021 kwa kudharau mahakama.
Alikataa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa mahakama kuhusu ufisadi wa serikali wakati akiwa uongozini kama rais.
Hukumu hiyo ilizua ghasia zilizosababisha vifo vya watu 350 na mamia ya biashara kuporwa na kuchomwa moto.