Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) inakaribia kutamatika huku macho yote yakielekezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kasarani, ambapo fainali kubwa itapigwa Jumamosi hii kati ya Madagascar na timu ya Morocco maarufu kama The Atlas Mountains.
Katika hatua ya nusu fainali iliyopigwa wiki hii, Morocco walionyesha ubabe wao kwa kuichapa Senegal (The Lions of Teranga) kwa mabao 2-0 katika mechi ya kuvutia iliyosheheni kasi na mbinu za hali ya juu. Madagascar kwa upande wao waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sudan, katika pambano la hali a juu.
Mashabiki kote barani Afrika macho sasa yako kwa mtanange huu unaotrajiwa wa kusisimua, Morocco wanasaka kuongeza heshima yao kama moja ya mataifa yenye historia ya mafanikio katika soka la Afrika, na Madagascar wakitafuta kutwaa taji lao la kwanza kabisa katika historia ya CHAN.
Kwa mwaka huu, Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) liliutangaza kuongezwa kwa mfuko wa zawadi hadi kufikia 1.3 bilioni ($10.4 milioni), ongezeko la asilimia 32 kutoka mashindano ya mwaka jana.Mshindi akitarajiwa kutia kibindoni [ millioni 452.2 ] wa pili akipata [millioni 155]na watatu akipata [millioni 90.4] wa nne akiondoka [millioni 77.5] vijana wa harambe stars watapokea millioni 25.5 kwa kushiriki katiaka michuano hiyo.



