VIONGOZI WA KIDINI NA WANAHARAKATI WAMTAKA WAZIRI WA USALAMA WA NDANI KIPCHUMBA MURKOMEN KUJIUZULU

0
37


‎Wakizungumza na vyombo vya habari mjini Mombasa, viongozi hao pamoja na wanaharakati walisikitishwa na matukio ya mara kwa mara kuhusu usalama nchini pasi na hatua mwafaka kuchukuliwa.

‎Makundi hayo yameghadhabishwa na tukio lililofanyika 25/1/2026 katika kaunti ya Nyeri ambapo kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua alishambuliwa alipokuwa akihudhuria misa ya jumapili katika kanisa la Witima ACK- Othaya,huku waumini wa kanisa hilo wakishambuliwa kwa vitoza machozi.

‎”Tunalaani vikali kitendo kilichofanyika jana,ambapo waumini pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa wameandamana na kinara wa DCP Rigathi Gachagua kushambuliwa na maofisa wa Polisi wakati wa Misa ya Jumapili katika kanisa la Witima ACK huko Othaya kaunti ya Nyeri” Walisema makundi hayo.

‎Kufuatia vurugu hizo makundi hayo sasa yanasisitiza maofisa wa usalama kutokaribia majengo ya kuabudu na badala yake wakae umbali wa mita 600 wakisema, visa hivyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara pasi na tume ya kushughulikia utendakazi wa Polisi IPOA kutochukua hatua kwa uharaka kuona wahalifu wanashitakiwa na kukabiliwa vilivyo kwa mjibu wa katiba.

‎”Tunatoa taarifa kwa maofisa wa Polisi kukaa umbali wa mita 6 katika majengo ya kuabudu, na iwapo mtu ni mhalifu fuateni sheria sio kuharibu ibada na kuhangaisha waumini” Walisisitika makundi hayo.

‎Vilevile makundi hayo yameitaka kamati ya kushughulikia usalama bungeni kuwahoji Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen pamoja na Mkuu wa Polisi Douglas Kanja miongoni mwa viongozi wa usalama kaunti ya Nyeri kulikofanyika vurugu hizo na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika na vurugu hizo.

‎”Tunaiomba kamati ya usalama bungeni kuwaita na kuwahoji viongozi wa usalama wakiongozwa na waziri Murkomen,Mkuu wa Polisi Douglas Kanja na viongozi wote wa usalama eneo hilo kwani wamekiuka maadili ya kikatiba na wachukuliwe hatua kali za kisheria”.Walisisitika makundi hayo.

‎Hatua ya makundi hayo kulaani vurugu hilo inajiri baada ya aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua kushambuliwa mara kwa mara wakati akihudhuria ibada na misafara yake kushambuliwa, hali inayozua hofu na udhibiti wa usalama wa taifa.

‎Simon (Cephas) Mwalimu.

LEAVE A REPLY