Ni Nani Aliye na Njama Fiche Wenye Uajiri wa Makurutu wa Polisi

0
125

‎Mvutano unaoonekana kati ya idara ya usimamizi wa polisi ya kitaifa na ofisi ya inspekta mkuu wa polisi ambapo kukiwa na utata juu ya nani ana mamlaka ya kuajiri na kusimamia makurutu si swala dogo, wala si jambo la kupuuzwa. Swala hili linastahili kuangaliwa kwa kina, bila kupendelea upande mmoja, bali kwa kujifunza ni nani anayesukuma, ni nani aliye nyuma ya pazia, na ni nani aliye na mpango fiche.

‎Kwa upande mmoja, kuna hoja ya msingi ya uwajibikaji wa katiba: Katiba ya Kenya imeweka wazi eneo la mamlaka za kuajiri, kusimamia rasilimali watu na kuhakikisha uwazi. Tukumbuke kwamba kiwango kinachowokezwa katika sekta ya usalama hasa uajiri wa makurutu – ni kiasi kikubwa cha pesa, mara nyingi mabillioni, na hivyo ni lazima wazi nani anaamua, ni vigezo gani vinatumika, na je mchakato unasimamiwa kikamilifu.

‎Inazua maswali makubwa kwamba kutatizana ni nani anafaa kuajiri makurutu, kuingia katika huduma ya polisi si jambo la kukimbizana hapa na pale kwenda kortini. Kuna watu ambao wanatazamia wana nafasi ya kutambuliwa, wana matumaini, wana hamu wanajiandaa kwa utaratibu. Hivyo nauliza: ni nani ako nyuma? Ni nani anayesukuma upendeleo? Ni nani yuko nyuma ya pazia inayoonekana wazi lakini haioniwi?

‎Katika kesi iliyoshughulikiwa na mahakama, kwa mfano, Mahakama ya Juu (High Court) ilitoa uamuzi wa kusimamisha uajiri wa makurutu 10,000 kwa sababu ya kipaumbele cha kesi ya kiKatiba kuhusu nani anayo mamlaka ya kuajiri.

‎Pia, mahakama ilikuta kwamba tangazo la uajiri lililotolewa na NPSC lilikuwa halikufuata taratibu za Katiba. Hii inaonesha kuwa si tu suala la muda bali suala la mamlaka halisi, muundo wa utawala, uwazi wa mchakato, na heshima ya Katiba yote

‎Kwa vijana wengi wanaotarajia kujiunga na huduma ya polisi, kusubiri kwa mwaka hadi mwingine bila mafanikio hakika kuna athari za kiakili, kisaikolojia na kijamii wanajiandaa, wanaandaa elimu, wanataka fursa. Hivyo, sasa hadi lini mchezo huu utaendelea?

‎Kwa taifa hili, huduma ya polisi ni uti wa mgongo wa utawala wa sheria, usalama na amani. Inawezekana kwa utata huu kuathiri ufanisi wa NPS haki ya raia kushirikishwa sawa, usawa katika uajiri, na kuondoa utata kuhusu nani ndiye anasimamia.

LEAVE A REPLY