Mfumo Wa E Procument Utasaidia, Ama ni Porojo?

1
178

Rais William Ruto, katika juhudi zake za kuimarisha uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha za umma, ametangaza mfumo mpya wa e-procurement. Mfumo huu unalenga kuwezesha utoaji wa kandarasi za serikali kufanyika kidijitali, kwa njia ya uwazi na bila upendeleo. Bila shaka, huu ni mwelekeo mzuri unaopaswa kuungwa mkono na kila mzalendo kwa kuzingatia kwamba upatikanaji wa kandarasi umekuwa ndio chanzo kikuu cha ufisadi hapa nchini

Nitasema hivi, kwamba kwa miaka miangi Kandarasi zimekuwa zikitolewa kwa misingi ya ukabila, rushwa, na urafiki wa kisiasa badala ya ushindani wa haki. Matokeo yake yamekuwa ni miradi hewa, ubadhirifu wa mabilioni ya pesa, na huduma duni kwa wananchi.

Kile ambacho wakenya wanahofia ni kwamba isiwe ikawa ni mfumo unaundwa kwa ulaghai mwingine wa ubadhilifu na ufisadi , tumeshuhudia mifumo mikubwa mingine kam e citizen iliyodhamiriwa kufanya huduma za seikali kuwa rais ukiingiwa na wakora na kuchafua huduma hiyo sio hiyo tu juzi tu mfumo wa SHA umechafuka.

Maswali mengi ambayo sasa tunajiuliza ni kwamba , serikali iko tayari kwa uwekezaji wa kutosha katika miundombinu ya kidijitali kuhakikisha mfumo huu unafanya kazi kwa ufanisi katika ngazi zote – kuanzia serikali kuu hadi kaunti?

Je, kuna mfumo madhubuti wa usimamizi na ufuatiliaji ambao utawekwa ili kuhakikisha kuwa taarifa zote za zabuni zinapatikana kwa wakati na kwa uwazi?

Itakuwaje kwa wafanyabiashara wadogo na wa kawaida ambao huenda hawana ujuzi wa kutumia mifumo ya kidijitali? Je, serikali ina mpango wa kuwajengea uwezo?

Je, ni hatua gani zimewekwa kuhakikisha kuwa maafisa wa serikali hawatatafuta njia za kukwepa mfumo huu, kama ilivyo kawaida katika baadhi ya taasisi za umma?

Ni adhabu gani zitakazowekwa kwa wale watakaobainika kukiuka sheria za e-procurement?
Kwa kweli, mfumo huu ukitekelezwa ipasavyo, unaweza kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya ununuzi wa serikali na kupunguza kwa kiwango kikubwa ufisadi. Lakini mafanikio yake yatategemea dhamira ya kweli ya viongozi wetu kuufanikisha bila kuupotosha.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY